Asilimia 96 ya waliofanya mtihani Shule Kuu ya Sheria mwaka 2022 hawajafaulu

0
33

Wanasheria na wadau mbalimbali wametaka utafiti ufanyike kubaini chanzo cha anguko kubwa la wanafunzi kwenye mtihani wa uwakili katika Shule Kuu ya Sheria Tanzania (LST) baada ya matokeo mabaya kupindukia katika mtihani uliofanywa mwaka huu.

Katika mtihani huo ambao ulifanywa na wanafunzi 633, wanafunzi 26 sawa na asilimia 4.1 pekee ndio wamefaulu mtihani huo, wanafunzi 342 wametakiwa kurudia baadhi ya masomo (suplimentary) huku 265 (asilimia 41.9) wakifeli na kukatishwa masomo.

Aidha, uongozi wa shule hiyo umejibu malalamiko ya wadau ukifafanua changamoto zilizopo ikiwemo maandalizi duni waliyoyapata wanafunzi hao katika vyuo vikuu walivyosomea shahada zao.

Afikishwa mahakamani kwa kuwadhalilisha marais wastaafu Tiktok

Naye Jaji wa Mahakama Kuu, Gabriel Malata amesema jawabu la changamoto zote zinazoikabili litapatikana iwapo utafanyika utafiti na kwamba si vema mwanafunzi kukwama miaka kadhaa katika Shule Kuu ya Sheria mara baada ya kumaliza shahada.

Katika mwaka wa masomo 2018/2019 kati ya wanafunzi 1,735 waliofanya mtihani, 347 (asilimia 20) walifaulu, 484 walirudia mtihani, huku 468 walifeli.

Vivyo hivyo 2016/17 na 2017/18 kati ya wanafunzi 2,662 waliofanya mtihani, 445 (asilimia 16.72) walifaulu, 1,611 (asilimia 60.53) walirudia mtihani na 606 (asilimia 22.76) walifeli.

Chanzo: Mwananchi.

Send this to a friend