Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imepeleka pendekezo kwa Serikali kuomba kupandishwa bei ya kipimo cha vinasaba, bei ambayo itahusisha gharama ya upimaji wa vinasaba kwa ajili ya sababu za kijamii, ikiwemo ya ugunduzi wa uhalali wa mtoto kwa wazazi husika.
Hayo yameelezwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt, Fidelis Mafumiko alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa bajeti na mwelekeo wa mamlaka hiyo jijini Dodoma.
Benki ya Dunia yaipa Tanzania trilioni 4.9
Ameeleza kuwa mapendekezo hayo yanalenga kusaidia kutoa huduma bila kuathiri shughuli za mamlaka hiyo, huku akieleza kuwa sampuli za kijinai zitakwenda kulingana na vigezo vilivyowekwa.
“Ukiacha sababu za kijinai, tuchukulie labda unataka kupima vinasaba vya mtoto, baba na mama ni shilingi 300,000 lakini hata yenyewe tumepeleka mapendekezo iongezwe kidogo kwa sababu ni ghali,” amesema.
Dkt. Mafuniko amebainisha sababu za pendelezo hilo ni kutokana na bei ghali ya ununuzi wa kemikali ambapo moja ya kupima vinasaba ambayo Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali hununua kwa kipindi cha miezi mitatu ni dola 6,000 [sawa na wastani wa TZS milioni 14].