BRELA: Kalynda ilipewa leseni ya kuuza vifaa vya kielektroniki

0
31

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imesema leseni ya kampuni iitwayo Kalynda E- Commerce Limited iliyotolewa Juni 21, 2022 ni kwa ajili ya uuzaji wa jumla wa vifaa vya kielektroniki na mawasiliano pamoja na ufanyaji wa biashara ya kiteknolojia ya kimataifa mtandaoni.

BRELA imesema kumekuwa na taarifa zinazoleta taharuki kuhusu kampuni hiyo kufanya biashara ya upatu ya kukusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa ahadi ya kupata faida ndani ya muda flani kinyume na bidhaa au huduma iliyoombewa leseni.

Taarifa ya BRELA imesema leseni ya biashara ya Kalynda E- Commerce Limited inamruhusu kufanya biashara ya masoko na mauzo ya bidhaa kwa njia ya mtandao pekee, hivyo ufanyaji wa biashara kinyume na leseni iliyotolewa ni kosa la jinai chini ya kifungu cha 19 cha sheria ya leseni za biashara, Sura Na. 208.

Ishara 7 zinazoonesha unatapeliwa katika biashara za kuwekeza

Aidha, Wakala imetoa angalizo kwa umma kuwa kabla ya kuingia kwenye mahusiano ya kibiashara na kampuni yoyote ni vema kupata uthibitisho wa uhalali na uwepo wa kampuni hiyo pamoja na biashara husika kutoka BRELA na mamlaka nyingine za Serikali.

Send this to a friend