Takwimu iliyotolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima imeonesha wastani wa watoto 491 wanabakwa na 93 wanalawitiwa kila mwezi.
Ameeleza kuwa asilimia 60 ya matukio hayo yanafanywa na ndugu wa karibu wa watoto husika huku matukio mengi yakiwa hayaripotiwi.
Wazazi wawatishia kifo watoto wao endapo watafaulu mtihani wa darasa la saba
Dkt. Gwajima ameyabainisha hayo wakati akizindua jengo la kikundi cha Sauti ya Jamii Kipunguni kinachojishughulisha na masuala ya kijamii ikiwemo kukemea vitendo vya kikatili, jijini Dar es Salaam.
Amesema “zaidi ya nusu ya watoto wamebakwa na kulawitiwa majumbani kwao na ndugu zao, asilimia 40 ndiyo wamefanyiwa ukatili nje ya nyumbani ama wakielekea shuleni, wakiwa shuleni au wakiwa wanarudi nyumbani. Hawa walioripoti ni asilimia 12 tu, wengi hawakuripoti.”
Aidha amesema kamati za jamii za ulinzi dhidi ya ukatili zilizoundwa mwaka 2017 zinaendelea kufanya kazi kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa.