Aina ya moshi unaotoka kwenye gari lako na unachoashiria

0
24

Unapoona moshi kwenye gari lako usio wa kawaida unapaswa kujiuliza maswali na kuchukua tahadhari. Kuna aina za moshi ambazo zikitoka kwenye gari lako huashiria tatizo kwenye moja ya mifumo ya ndani ya gari.

Hii ni aina ya moshi na jinsi inavyoashiria;

Moshi mweupe
Moshi mweupe kama mawingu mara nyingi huonekana asubuhi pale unapokuwa unaliwasha gari au linapokuwa limeachwa nje na mvua imenyesha. Unapoona moshi huu ujue mfumo wa upoozaji umepooza injini kupita kiwango kinachohitajika, hivyo kusababisha kutoa moshi mweupe.

Unachotakiwa kufanya, liwashe gari lako kisha liache kwa muda wa dakika 5 mpaka 10 lichemke baada ya hapo anza safari yako.

Moshi wa kijivu
Moshi huu husababishwa na mambo kadhaa ikiwemo ‘Pcv valve’ kushindwa kufanya kazi vizuri, oil kuingia kwenye sehemu isiyo sahihi, inavuja au oil kuwa nyepesi. Kama unatumia gari la ‘automatic’ na umeona moshi wa kijivu inamaanisha ‘transmition fluid’ imepungua kwenye ‘gear box’, kwa maana hiyo inawezekana kuna mahali oil sili zinavuja, hivyo unapaswa kulipeleka kwa fundi likaguliwe.

Njia 5 za kuepuka kutapika safarini

Moshi wa bluu
Moshi huu unapotoka unaashiria kuwa oil inavujia ndani ya injini. Kama gari lako limefanyiwa ‘service’ hivi karibuni, inawezekana injini oil imejazwa kupita kipimo kinachotakiwa hivyo kusababisha presha ndani ya injini kuzidi na oil kuvuja.

Pia inawezekana kuna mahali ‘gasket’ zimeisha au zinaachia na kusababisha oil kuingia sehemu ambayo siyo sahihi.

Unapopata tatizo hilii hakikisha unapima oil kwa kutumia ‘deep stick’ kubaini kiwango cha oil inayopotea au peleka kwa fundi kwa msaada zaidi.

Moshi mweusi
Moshi mweusi humaanisha kuwa gari linachoma mafuta mengi kupita kiasi na ili kutatua tatizo hili unatakiwa kuweka filter mpya.

Chanzo: Mwananchi