Tanzania imepata mkopo wa gharama nafuu wa TZS bilioni 310 kutoka Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa ajili ya upanuzi wa mfumo wa utambuzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na uendelezaji na utunzaji wa mfumo wa taarifa za ardhi.
Hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo baina ya Serikali ya Tanza na Korea Kusini itakayotolewa kupitia benki ya Exim ya Korea, imefanyika leo Oktoba 27, 2022 katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Korea Kusini iliyopo Seoul.
Mabehewa 36 ya SGR kuwasili nchini kuanzia Novemba 10
Mkataba wa awamu ya pili wa mradi wa upanuzi wa mfumo wa utambuzi wa NIDA una thamani ya TZS bilioni 161 na mkataba wa uendelezaji na utunzaji wa mfumo wa taarifa za ardhi ambao una thamani ya TZS bilioni 149.
Akizungumza wakati wa halfa hiyo iliyoshuhudiwa na Waziri Mkuu wa Korea Han Duck-Soo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Tanzania na Korea zinajivunia mahusiano yaliyodumu kwa miaka 30 ambayo yamekuwa chachu katika kukuza uchumi wa nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali.
Amesema kuwa kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Korea (EDCF), Tanzania imeweza kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo madaraja, barabara, kituo cha kisasa cha kusajili meli cha Zanzibar, njia ya kusafirishia umeme, hospitali ya Mlonganzila, mradi wa umwagiliaji uliopo Zanzibar na utoaji huduma wa vitambilisho vya Taifa.