Kelele za muziki wa kanisa zadaiwa kusababisha maradhi ya moyo kwa mama anayeishi jirani

0
18

Wakazi wa mtaa wa Mlimani mkoani Arusha wamelalamikia Kanisa la Nguvu ya Utimilifu kupiga vyombo vya muziki kwa sauti kubwa na bila mpangilio nyakati za usiku hali inayowasababishia kero.

Wananchi wa eneo hilo wamedai kitendo hicho kimekuwa kikiendelea kwa muda wa miaka mitatu sasa licha ya kuketi vikao vinne na kanisa hilo katika uongozi wa mtaa, kata na Wilaya na kwamba Mkuu wa Wilaya aliwataka Baraza la Uhifadhi wa Mazingira la Taifa (NEMC) Kanda ya Kaskazini kumaliza tatizo hilo lakini hakuna utekelezaji wowote.

Mmoja wa wakazi wa mtaa huo, Malijani Mustafa amesema upigaji mbovu wa vyombo umesababisha mama mmoja kupata maradhi ya moyo, na kuiomba Serikali kuwahamisha eneo hilo la makazi na kuwapatia eneo lingine.

Papa Francis awaonya makasisi na watawa wanaotazama video za ngono

Naye Meneja wa NEMC Kanda ya Kaskazini, Lewis Nzali amesema waliandika barua kwenda kwa kanisa hilo ili lijirekebishe na kuongeza kuwa kila akituma wataalamu hakuti kelele zinazodaiwa.

Ameongeza kuwa taasisi au mtu binafsi mwenye tabia kama ya kanisa hilo akifikishwa mahakamani sheria itampa adhabu ya kifungo cha miaka saba gerezani au kulipa faini ya shilingi milioni tano.

Mchungaji Msaidizi wa Kanisa hilo, Jackson Ibrahim amekana kupiga vyombo kwa sauti ya juu na kudai kuwa hata NEMC ilipofika kanisani hapo hawakukuta kelele.

Send this to a friend