Tanzania ya pili Afrika utoaji chanjo ya UVIKO-19

0
29

Tanzania imeshika nafasi ya 2 kwa kiwango cha juu cha uchanjaji wa chanjo ya UVIKO-19 huku ikiwa imefikia asilimia 37.9 ya uchanjaji wa wananchi kwa mujibu wa takwimu za kidunia.

Hayo yamebainishwa na Mratibu Kiongozi wa Kimataifa wa Ubia wa Utoaji wa chanjo ya UVIKO-19, Ted Chaiban ambapo ameipongeza Tanzania na nchi nyingine barani Afrika pamoja na wadau wa Sekta ya afya kwa uhamasishaji na kuchanja wananchi chanjo dhidi ya janga hilo.

Walimu waongoza kwa utoro kwa asilimia 66.5

Naye Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, wadau wa maendeleo, watumishi wa afya na watu wengine waliowezesha kufanikisha jitihada hizo za kuwakinga wananchi dhidi ya UVIKO-19 na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya 2 Afrika kwa kiwango cha juu cha uchanjaji.

Send this to a friend