Mabasi 750 ya Mwendokasi kupelekwa Mbagala

0
22

Mkurugenzi wa Maendeleo ya  Usafirishaji wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), Fanuel Karugendo amesema mabasi 750 yaendayo haraka yanatarajiwa kuanza kufanya kazi katika barabara ya Mbagala jijini Dar es Salaam Machi 2023.

Ameyasema hayo  leo Jumamosi Oktoba 29, 2022 wakati akishiriki kufanya usafi pamoja  na wakazi wa Mbagala na wadau wengine katika Kata ya Mbagala.

Karugendo amesema mradi huo unatarajiwa kuanza na mabasi 750 kutokana na wingi wa watu katika eneo hilo ambao pia utasaidia kusafirisha abiria 600,000 mpaka 700,000 kwa siku.

“Hata katika kuja kushiriki usafi leo ni katika kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kujiandaa na ujio wa mabasi hayo ambayo asili yake ni kutoa huduma katika mazingira safi,” amesema.