Dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo hususani miguu na mikono kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.
Matatizo haya ya kiafya husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika.
Hizi ni sababu zinazoweza kusababisha viashiria vya ganzi;
Kukaa mahali kwa muda mrefu
Ulalo usio rafiki na kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu huweza kugandamiza au kubana mishipa ya fahamu ambayo ndio yenye kupokea misisimko ya mfumo wa fahamu.
Kupata majeraha
Kupata majeraha katika mgongo au kiuno ambako ndio mishipa mingi ya fahamu inachomoza katika uti wa mgongo ni sababu moja wapo ya kupata ganzi.
Pia uwepo wa mgandamizo unaoleta shinikizo katika mishipa ya fahamu inayotokea katika uti wa mgongo, mfano santuri za mgongo zinapochoropoka au kuhama.
Mishipa ya fahamu inaweza kuathirika kutokana na uvutaji tumbaku, unywaji pombe, matibabu ya therapy na mionzi.
Wanawake Geita walalamika kuingiliwa kimwili na Popobawa usiku (video)
Upungufu wa vitamin B mwilini
Hii ni moja ya sababu ya mara kwa mara inayochangia kupata tatizo hili hasa kwa watu wenye umri mkubwa ambao miili yao ufanisi umepungua.
Upungufu wa damu
Damu kuwa chache au kutofikia sehemu fulani ya mwili kutokana na kujeruhiwa au kutokana na mishipa ya damu kuharibika.
Kukosa mtawanyo wa damu katika maeneo ambayo mishipa ya damu imeharibika kutokana na mrundikano wa mafuta mabaya au au kutokana na kupata shambulizi.
Magonjwa
Kuugua magonjwa kama vile sukari, kiharusi au kiharusi kilichotokana na kuziba kwa mishipa ya damu, mishipa ya damu kuharibika, kifafa au degedege, matatizo ya tezi ya shingo na uvimbe katika ubongo.