Meridianbet yawashika mkono Hospitali ya Tumbi

0
32

Kampuni ya Meridianbet iliyoambatana na timu nzima ya masoko, akiwemo meneja masoko wa kampuni hiyo Ndugu Matina Nkurlu, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Maudhui Bw Twaha Ibrahimu, leo Novemba 11, 2022 ilitembelea Hospital ya Rufaa ya Tumbi mkoa wa Pwani, kwaajili ya kutoa msaada wa vifaa kwa matumizi ya wagonjwa katika hospitali hiyo.

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Afya chini ya Waziri mwenye dhamana hiyo Mhe Ummy Mwalimu, Meridianbet iliguswa na mahitaji ya hospital hiyo na hivyo waliamua kuchangia neti, barakoa na vifaa vingine ikiwa ni sehemu ya utamaduni wao wa kurudisha kwa jamii kile kidogo wanachokipata.

Meridianbet pamoja na uongozi wa Hospitali ya Tumbi walishiriki owa pamoja katika zoezi hilo la kukabidhiana vifaa hivyo, na mara ya kukamilika kwa zoezi la kutoa msaada huo, mwakilishi kutoka Hospitali hiyo, Christina Salusi alitoa shukrani zake kwa kampuni ya Meridianbet kwa msaada huo.

“Kwa niaba ya Uongozi na Menejimenti nzima ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, napenda kuwashukuru kampuni ya Meridianbet kwa kuguswa na kuamua kutoa msaada huu mkubwa wa vifaa vya matibabu, hakika hili ni jambo kubwa kwetu na kwa jamii nzima” alisema Christina Salusi- Muuguzi.

Aidha timu nzima ya Meridianbet walioambatana na Meneja Masoko Matina Nkurlu hawakusita kuzungumza kile kilichowasukuma kutoa msaada huo tena kwa mara ya kwanza kwa Hospitali ya Mkoa wa Pwani-Tumbi.

“Sisi kama Meridianbet huwa tuna utamaduni wa kutoa kwa jamii kile kidogo tulichopata kama faida kwenye biashara yetu, na hii sio mara ya kwanza tumewahi kufanya kwenye hospitali ya Mwananyamala, Amana n.k

“Na tumeamua kuja hapa Hospitali ya Tumbi ili kuwashika mkono katika juhudi zenu za kuokoa maisha ya wapendwa wetu, hivyo tunawaahidi kuendelea kushirikiana nanyi” Twaha Ibrahimu

Hata hivyo, Muuguzi ndugu Salusi alitoa nafasi ya wawakilishibwa Meridianbet kutembelea baadhi ya maeneo katika Hospitali hiyo ili kuwajulia hali wagonjwa waliofika kutibiwa.  Moja ya eneo lililotembelewa ni wodi ya wajawazito ambao  nao hawakusita kutoa neno lao kwa kampuni  hiyo namba moja Tanzania na Afrika Mashariki kwa michezo ya kubashiri kutokana na msaada huo.

Mmoja ya wazazi waliojifungua katika hospitali hiyo, Bi Zuwena Rashi mara baada ya kupokea msaada huo hakusita kuonesha hisia zake za furaha.

“Kwakweli mimi kama mzazi nimefurahishwa na hiki mlichokifanya kwetu, nawashukuru sana kampuni ya Meridianbet kwa kugusa maisha yetu, hususani ya mama wajawazito na wagonjwa wengine, msaada huu utasaidia wagonjwa wengi wanaotibiwa kwenye Hospitali ya Tumbi” -Zuwena Rashid

Kampuni ya Meridianbet inapenda kuushukuru Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, Mkoa wa Pwani, kwa ushirikiano wao walioutoa mwanzo wa zoezi mpaka mwisho, na unapongeza juhudi zinazofanywa na Hospitali hiyo kuokoa maisha ya watanzania wengi na kurejesha matumaini zaidi. Unaweza kubeti Meridianbet kwa dau dogo la kuanzia TZS 250/= kwa kupiga *149*10#.

 

Mbali na michezo ya kubashiri, pia Meridianbet wana michezo mingine mingi ya kasino mtandaoni, unaweza kucheza mchezo wa Aviator ukawa rubani wa maisha yako, kuna mchezo wa Roulette, Poker, n.k. Pia Kampuni hiyo inaendesha promosheni kibao ya michezo ya kubashiri, ambapo unaweza kujishindia Bajaji droo hii itatangazwa Novemba 22 mwaka huu, lakini pia kuna promosheni ya SHINDA TV ya Inchi 50 kubeti kwa USSD Code.

Send this to a friend