TRA: Hatukusanyi kodi kwa mabavu tena
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Uledi Mussa amesema kitengo cha ‘task force’ kilichokuwapo huko nyuma kimeondolewa na sasa wanakusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara bila kutumia mabavu.
Mussa amesema hayo leo Jumanne Novemba 15, 2022 katika kikao baina ya TRA na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) jijini Dar es Salaam.
Precision Air yaanza taratibu za kuwalipa waathirika wa ajali
“Kwa sasa tunakusanya mapato bila mabavu. Waachane kabisa kabisa na matumizi ya mabavu. Tunataka walipa kodi wajisikie vizuri kabisa. Hatuna tena Task Force (kikosi kazi),” amesema.
Aidha, Mwenyekiti huyo amesema kwa sasa wanawaangalia kwa ukaribu walipa kodi ili kuhakikisha wanaendelea kufanya biashara zao vizuri na pia wawe walipa kodi siku zijazo.
Amesema hatua hiyo imewezesha ukusanyaji wa mapato kuongezeka, akitolea mfano mapato ya Septemba yamevuka lengo badala ya kukusanya TZS trilioni 6.2 wamekusanya TZS trilioni 6.3.