Serikali imesema inafuatilia taarifa za kukamatwa kwa wasafiri saba wakiwemo wanne waliotoka Tanzania wakiwa na kilo 61 za dhahabu zenye thamani ya randi 320 milioni (TZS bilioni 9.18) katika Uwanja wa Ndege wa Mumbai nchini India.
Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara wa Tume ya Madini Tanzania (TMC), Venance Kasiki amesema wanaendeea kufanya uchunguzi kujiridhisha kama kweli madini hayo yametoka Tanzania ili kuliepusha taifa na utakatishaji wowote ambao unaweza kuwa umepangwa.
“Wao wanasema walipofika Doha walipewa madini hayo na mtu wasiyemjua, sasa inawezekanaje? Hadi sasa wanashikiliwa na vyombo vya usalama India,” amesema Kasiki.
Kasiki ameongeza kuwa endapo madini hayo yametoka nchini yatakuwa yamechenjuliwa na wachimbaji wakubwa kwani hakuna mchimbaji mdogo anayeweza kutorosha uzito huo.
Maofisa wa forodha waliwakamata wasafiri wanne waliokuwa wanatoka Tanzania wakiwa na kilo 53 za dhahabu zenye thamani ya randi milioni 281.7 (TZS bilioni 8.08) na wengine watatu waliokuwa wanatoka Dubai wakiwa na kilo nane za madini hayo.
TRA: Hatukusanyi kodi kwa mabavu tena
Taarifa zinasema dhahabu hiyo ilifichwa kwenye mikanda iliyotengenezwa na Falme za Kiarabu na walikabidhiwa na raia wa Sudan waliyekutana naye Uwanja wa Ndege wa Doha walikobadilisha ndege.