Tanzania yatoa maelekezo kwa Mabalozi wanaoiwakilisha nchi

0
26

Wawakilishi wa Tanzania katika nchi mbalimbali duniani wameelekezwa kuanzisha, kushawishi na kufuatilia mikataba yenye manufaa katika nchi zao za uwakilishi badala ya kusubiri mapendekezo kutoka kwa viongozi wa nchi husika.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa wiki moja uliowakutanisha wajumbe 45 wa Tanzania na viongozi wakuu wa Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Katika mkutano huo, wajumbe hao watapokea maagizo kutoka kwa viongozi wakuu wa nchi kwa ajili ya utekelezaji wa diplomasia ya uchumi wa nchi pamoja na kubadilishana uzoefu, kuorodhesha changamoto zao na kuweka mikakati ya utekelezaji kwa ufanisi wa majukumu yao.

Akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Dkt. Tax, Naibu waziri wa wizara hiyo, Mbarouk Nassor Mbarouk amesema wajumbe wana changamoto ya kuanzisha, kuonesha uwezo wa kujadiliana na kufanya mikataba yenye manufaa kwa nchi.

“Hatupaswi kusubiri mikataba na makubaliano kutoka kwa nchi zinazoandaa ili tutoe mapendekezo. Tunapaswa kuanzisha na kufuatilia kwa karibu utekelezaji,” amesema.

Serikali kufuatilia waliokamatwa na dhahabu India wakitokea Tanzania

Ameeleza kuwa sera ya mambo ya nje ya nchi ni kielelezo cha sera za ndani, hivyo kuwataka wajumbe kuendelea kuzingatia vipaumbele vya Taifa katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya nchi 2025, Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano na Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Send this to a friend