Jaji Mstaafu Joseph Warioba amesema alichokisema Mbunge Dkt. Bashiru Ally hakikuwa na shida yoyote kwa kuwa alikuwa akitoa hoja yake, na kwamba viongozi wanapaswa kujibu hoja hiyo badala ya kumshambulia.
Akizungumza na chombo kimoja cha habari nchini, Jaji Warioba amesema ni kweli Serikali inafanya kazi nzuri lakini hiyo haimaanishi kila kitu kisifiwe, endapo kuna hoja ambayo itahitaji kujadiliwa iangaliwe.
“Hawa ni viongozi wa nchi, mimi nilifikiri watakuwa wanatetea wananchi zaidi. Naona kama wanatetea Serikali zaidi. Mimi nadhani kama wanatofauti zao huko wasizifanye ni tofauti za kitaifa. [..] Mimi sioni kama tunasaidia nchi kuanza kusema huyu awajibike kwa sababu ya mawazo aliyotoa, hivi mtu akitoa mawazo yake imekuwa ni kosa?” amehoji
Warioba.
Tuhuma za rushwa zapelekea chaguzi CCM kuahirishwa
Aidha, Jaji Warioba amewakosoa wote wanaodharau nafasi yake ya ubunge kwa kuuita kuwa ni ubunge wa Ikulu, na kusema kuwa yeye ni mbunge kama wabunge wengine ambaye pia anatambulika kwenye katiba ya nchi, na kwamba hajateuliwa ili kuitetea Ikulu.
Dkt. Bashiru hivi karibuni alizungumza na wakulima wadogo katika warsha iliyoandaliwa na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) akiwasihi kuacha tabia ya kushukuru na kusifu viongozi badala yake wadai haki zao kwa viongozi wao.