Rais Samia: UWT fanyieni kazi suala la udhalilishaji dhidi ya watoto

0
36

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka wanachama wa Jumuiya ya Wanawake wa chama hicho (UWT) kuacha kuzungumza tu badala yake kulifanyia kazi suala la uzalilishaji dhidi ya watoto.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatatu Novemba 28, 2022 wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa uchanguzi wa UWT uliofanyika jijini Dodoma.

“Hatujasimama tukalifanyia kazi tunaliimba tu, tumeliimba kwenye makongamano yote tuliyokwenda, na mimi nikaelekeza nikasema wadhalilishaji jamani ni sisi wenyewe, kama hatulitaki tutasimama tuseme hili hatulitaki lakini kinachotokea ni nini namba za udhalilishaji zinakua,” amesema.

Rais mstaafu wa Comoro ahukumiwa kifungo cha maisha jela

Aidha, ameeleza kutoridhishwa na kasi ya kujiunga uanachama wa UWT na uendeshaji wa miradi yake ya kiuchumi ambapo ameeleza kuwa kuanzia mwaka 2017 hadi 2022 jumuiya hiyo imeingiza wanachama wapya 86,288 ambao amesema sio idadi nzuri kwao.

“Ukichukua idadi hiyo ukiigawa kwa mikoa 32 na kujua mikoa mengine ni midogo sana kama ile ya Zanzibar unapata wanachama 2697 tu sasa hii sio kazi nzuri sana,” amesema.

Akizungumzia upande wa miradi ya kiuchumi, Rais Samia ametoa wito kwa jumuiya kufanya miradi mikubwa itakayoipa Jumuiya nguvu ya kiuchumi kwa kuwa miradi inayoendeshwa na jumuiya hiyo mingi ni ya vibanda, mashine za kusaga na mingine midogo ambayo haijaipa nguvu kiuchumi UWT.

Send this to a friend