Nigeria kuzindua roboti wa Kiafrika anayezungumza Kiswahili

0
39

Nigeria inatarajia kuzindua roboti ya kwanza barani Afrika yenye sura ya binadamu iliyopewa jina la ‘Omeife’ leo Desemba 02, 2022 huko Abuja.

Roboti huyo ya kike ana urefu wa futi 6 kama binadamu, ameundwa na kampuni ya teknolojia ya Nigeria, kundi la Uniccon ambao ni mojawapo ya waanzishaji wa teknolojia inayokua kwa kasi zaidi nchini humo.

Mkurugenzi Mtendaji wa kikundi hicho, Chuks Ekwueme amesema Omeife ana uwezo wa kuzungumza lugha 8 tofauti zikiwemo Yoruba, Hausa, Igbo, Kifaransa, Kiarabu, Kiswahili, Pidgin, Wazobia Afrikaans na lugha ya Kiingereza.

Ndege ya Tanzania (Airbus A220) yashikiliwa Uholanzi

Roboti huyo alitambulishwa kwa mara ya kwanza huko GITEX, Dubai na Waziri wa Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali wa Nigeria, Isa Pantami huku akipongeza kujitolea kwa kundi hilo kutekeleza jukumu muhimu katika kuhimiza uvumbuzi barani Afrika.

Send this to a friend