Wakamatwa na vifaa vya wizi kutoka Bwawa la Nyerere

0
42

Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Rufiji linawashikilia watuhumiwa 65 kwa makosa mbalimbali wakiwepo wahalifu waliokamatwa na vifaa vya mradi wa umeme katika Bwawa la Mwalimu Nyerere.

Akitoa taarifa hiyo leo Desemba 7, 2022 Kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna Msadizi wa Polisi, ACP Protas Mutayoba amebainisha kuwa Jeshi hilo liliendesha operesheni kali katika mkoa huo na kufanikiwa kukamata mtungi wa gesi uliokuwa unakwenda katika mradi wa bwawa la Mwalimu Nyerere.

Aidha, Kamanda Mutayoba amesema Jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata watuhumiwa wa dawa za kulevya pamoja na pikipiki zinazotumika katika matukio ya uhalifu.

Wasanii wanaohamasisha uvutaji bangi kuwajibishwa

Katika tukio jingine Kamanda Mutayoba amesema jeshi hilo linamshikilia mtuhumiwa mmoja kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali na mitego ya kutegea wanyama, na kubainisha kuwa upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya taifa ya mashitaka kwa hatua zaidi.

Jeshi la Polisi limetoa rai kwa wananchi wote wa mkoa huo kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa jeshi hilo ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya walifu wote.

Send this to a friend