Hizi ni faida 9 za kula muhogo usizozijua

0
28

Muhogo ni chakula chenye mizizi mingi inayotumiwa sana katika nchi nyingi duniani. Inatoa virutubisho vingi muhimu, ikiwa ni pamoja na wanga, ambayo inaweza kuwa na manufaa ya afya.

Pengine wewe ni mpenzi wa kula mihogo lakini hufahamu maajabu yake. Hizi ni faidia 9 za muhogo katika afya ya binadamu;

1.Huboresha usagaji chakula
Muhogo una wanga mwingi ambao husaidia katika usagaji wa chakula.

2.Hudhibiti sukari
Kutokana na kuwa na nyuzinyuzi nyingi inasaidia kudhibiti viwango vya sukari ya damu, kupunguza viwango vya cholesterol ya damu na kuboresha afya ya utumbo kwa ujumla.

3.Husaidia kinga ya mwili
Muhogo ni chanzo kizuri cha vitamin C ambayo inaweza kukulinda na kusaidia utendaji kazi wa seli za kinga mwilini mwako.

4.Nzuri kwa ngozi
Kula mihogo inaweza kusaidia kulinda ngozi yako kuharibika na kuchochea uzalishaji wa collagen utakayoboresha ngozi yako.

5.Huondoa makovu na madoa
Maji ya muhogo yanaweza kusaidia katika uponyaji wa makovu ikiwa utapaka katika eneo lote lililoathiriwa walau mara mbili kwa siku.

6.Husaidia nywele kukua haraka
Mizizi na majani yake yanaweza kutumika kutengeneza unga ambao utautumia  kupaka kwenye nywele zilizotiwa mafuta saa moja kabla ya kuziosha. Kufanya hivi mara mbili kwa wiki kutaleta mabadiliko.

7.Huponya maumivu ya kichwa
Wengi wetu tunakabiliwa na maumivu ya kichwa. Lakini unaweza kutibu kwa msaada wa mihogo, unachohitaji ni kuchukua mizizi ya mihogo au majani yake na uyaloweke kwenye maji kwa masaa kadhaa. Tengeneza juisi safi kwa kutumia blenda na unywe mara mbili kwa siku.

8.Hutibu ugonjwa wa kuharisha
Muhogo hushughulikia hali kama vile kuharisha pia. Unaweza kuchukua vipande kadhaa vya mihogo na kuvichemsha, subiri hadi joto la kawaida. Kunywa mara mbili kwa siku.

9.Nzuri kwa macho
Muhogo una vitamini A kwa wingi ambavyo huboresha afya ya macho yako na katika siku zijazo huzuia upofu au kutoona vizuri.