Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amesema wizara bado inaendelea kuchunguza sakata la Hassan Mwakinyo baada ya kupoteza pambano lake nchini Uingereza.
Akizungumza katika mahojiano na Clouds 360 Mchengerwa amesema wamekuwa na utaratibu wa kufuatilia kila jambo linalotokea katika sekta ya Sanaa, Utamaduni na Michezo hivyo walipoona sintofahamu iliyotokea nchini Uingereza wameedelea kufuatilia kjua nini kilitokea.
“Nimefanya mazungumzo nilipokuwa kule Tanga na Mwakinyo, tumekubaliana tuonane ili tuweze kujua hasa kiundani kile ambacho kilitokea. Lakini pia hata yeye ana madai yake kadhaa ambayo aliniambia anatamani kuniona ili tuweze kuzumza,” amesema.
Alichosema Khadija Kopa kuhusu uhusiano wa Diamond na Zuchu
Aidha, amesema kama wizara iliyopewa dhamana ya kusimamia michezo hawachukulii jambo lolote kawaida, jukumu lao ni kuhakikisha wanafuatilia kila jambo ambalo haliko sawa linalotokea ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kwa kuwa ni nchi ndiyo inayowakilishwa.
Septemba 18, 2022 Bodi ya Ngumi za Kulipwa Uingereza (BBBC) lilimfungia bondia Hassan Mwakinyo kucheza ngumi nchini Uingereza siku chache baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Liam Smith kwa TKO raundi ya nne katika pambano lenye raundi 12 na kudai sababu za kupoteza mchezo huo ni baada ya kupoteza begi lake na kupewa viatu ambavyo havikumfaa.