Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa kilimo

0
23

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa kilimo utakaohusisha viongozi, watu mashuhuri na wadau wapya takribani 3,000.

Uamuzi huo umetangazwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn katika Jukwaa la Mtandao wa Chakula Afrika (AGRF) nchini Marekani, ambapo Rais Dkt. Samia amesema anatarajia mkutano huo utaendeleza uimarishaji wa mifumo ya chakula na kilimo katika vipaumbele vya Serikali, kupeana taarifa na kutumia teknolojia ya kisasa kwa ajili ya mifumo imara ya chakula.

Ameongeza kuwa wageni mbalimbali watakaohudhuria mkutano huo wataweza kujadili namna ya kuimarisha biashara miongoni mwa miji mbalimbali ili kuchangia usalama wa chakula, ukuaji na uvumilivu.

Lengo lingine ni kushawishi nchi zote juu ya ajira kwa vijana ambapo kila nchi barani Afrika itaweka wazi mikakati yake ya malengo ya ajira hizo na namna ya kufanikisha.

Katika kuimarisha shughuli za kilimo serikali ya Tanzania imeongeza bajeti yake karibu mara nne katika sekta hiyo kutoka dola za Kimarekani milioni 126.7 kwa mwaka 2021/2022 hadi dola milioni 411.2 mwaka 2022/2023.

Send this to a friend