Polisi katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels, wamewakamata takribani mashabiki 100 wa soka kufuatia kushindwa kwa Morocco dhidi ya Ufaransa katika nusu fainali ya Kombe la Dunia.
Miongoni mwa mashabiki waliozuiliwa Jumatano usiku walikuwa watu wanaoshutumiwa kwa kuvuruga utulivu wa umma, kuharibu magari mawili ya polisi na kumiliki silaha zisizoruhusiwa.
Messi atangaza fainali ya Kombe la Dunia kuwa mchezo wake wa mwisho
Baadhi ya mashabiki walikuwa wamejifunika bendera za Morocco na walipambana kwa muda mfupi na polisi katikati mwa Brussels baada ya Morocco kufungwa 2-0 na Ufaransa.
Mashabiki hao, walikusanyika karibu na kituo cha Brussels South na kurusha fataki na vitu vingine kwa polisi pamoja na kuwasha baadhi ya mifuko ya taka huku polisi wakijibu kwa kutumia maji ya kuwasha na mabomu ya machozi.