Mchungaji afariki baada ya kufunga kwa siku 8 bila kula

0
62

Mchungaji wa kanisa ambalo halijafahamika Abdiel Raphael (42) mkazia wa Mtaa wa Uwanja kata ya Nyankumbu mkoani Geita amefariki dunia kwa njaa baada ya kufunga kwa maombi maalumu kwa mda wa siku nane bila kula huku akiwaambia waumini wake kuwa akifa atafufuka kama Yesu.

Kamanda wa Jeshi polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema mchungaji huyo alifariki Disemba 3, 2022 akiwa ndani kwake.

“Alikuwa anawaaminisha waumini wake kwamba anao uwezo wa kufa na kufufuka, anao uwezo wa kuishi bila kula kama Yesu na bado akifa na atafufuka.

Waumini wa kanisa hilo baada ya kugundua amefariki Disemba 3, 2022 walisubiria afufuke kama alivyowaambia lakini ilipofika Disemba 9, 2022 harufu ya mwili huo ilikuwa kali ndipo wakaamua kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa.

Waumini hao wamesema mchungaji huyo aliwaambia kabla ya kuanza kufunga endapo wakisik

Send this to a friend