Multichoice yaamriwa kuwalipa Simbu na wenzake TZS milioni 450

0
24

Nyota watatu wa riadha nchini wameshinda kesi baada ya Mahakama ya Wilaya ya Arusha kuitaka Kampuni ya Multichoice kuwalipa fidia ya TZS milioni 450 kwa kutumia picha za sura zao katika matangazo ya kibiashara bila ridhaa yao.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya kesi ya madai iliyofunguliwa na wanariadha hao Alphonce Simbu, Failuna Abdi na Gabriel Geay ya kutumiwa kwa picha zao katika matangazo ya kibiashara bila ridhaa yao.

Msichana ahukumiwa jela kwa kosa la kumbusu mwanaume

Pamoja na kiasi hicho cha fidia, kila mmoja atalipwa TZS milioni 150 ikiwa ni pamoja na riba ya asilimia 25 ya kiasi hicho kuanzia tarehe waliyofungua kesi hiyo hadi tarehe ya hukumu, pia riba ya asilimia 10 ya kiasi hicho cha fidia kuanzia tarehe ya hukumu hadi tarehe ya kumaliza malipo yote.

Hakimu Bittony Mwakisu amesisitiza kuwa lazima ifahamike picha ya mwanamichezo ni rasilimali inayoonesha thamani ya kibiashara ambayo inaweza kumwingizia kipato, na hakuna mtu anayeweza kunufaika nazo isivyo halali bila wanamichezo kuwa sehemu ya manufaa hayo.

Send this to a friend