Wafunga ndoa wakiwa wamevalia jezi ya Argentina na Ufaransa

0
77

Wanandoa wanaoishi Kerala nchini India, Sachin na Athira wamewashangaza watu baada ya kufunga ndoa siku ya fainali za Kombe la Dunia la FIFA wakiwa wamevalia jezi kuonesha mapenzi yao kwa timu hizo.

Ingawa Sachin na Athira walikubaliana juu ya mambo mengi kuhusu siku yao maalum, jambo moja ambalo hawakuafikiana ni kuhusu timu ambayo kila mmoja aliiunga mkono.

Sachin ni shabiki mkubwa wa Argentina na alivalia jezi ya  nahodha wake Lionel Messi huku Athira shabiki mkubwa wa timu ya Ufaransa na yeye alivalia jezi ya mshambuliaji Kylian Mbappe.

Saa chache kabla ya timu hizo mbili kukutana katika Uwanja wa Lusail nchini Qatar katika moja ya mechi kali katika historia ya Kombe la Dunia 2022, walifunga ndoa katika sherehe iliyofanyika katika jiji la Kochi.

Orodha ya filamu 10 bora za mwaka 2022

Inaripotiwa kuwa baada sherehe ya harusi yao, wanandoa hao waliondoka haraka katika karamu ya harusi ili kurejea nyumbani kwa Sachin huko Thiruvananthapuram umbali wa kilomita 206 (maili 128) ili kutazama fainali iliyoibuka kuwa ya kusisimua.

Baada ya ushindi wa Argentina kwa penati 4-2 Jimbo la Kerala ambako Messi ana wafuasi wengi, wamekuwa akisherehekea ushindi huo tangu Jumapili usiku huku mashabiki wakipeperusha bendera za Argentina na kufyatua fataki katika jimbo zima.

Send this to a friend