Wazee wa Yanga watishia kutonunua bidhaa za Azam kisa Fei Toto
Wazee wa Klabu ya Young African na viongozi wa matawi wamewaomba viongozi wa klabu hiyo kufanya utafiti kuhusu Azam FC kuhusika katika sakata la Feisal Salkum kutaka na iwapo watabaini ni kweli waweze kuvunja mkataba walio nao wa kuwatangazia bidhaa zao.
Hayo yameeleza leo wakati wakizungumza na waandishi wa habari na kudai kuwa Azam ambao ni wadhamini wa Yanga wanaushirikiano wa kibiashara hivyo iwapo madai hayo ni kweli klabu hiyo kupambana na Azam ni ngumu isipokuwa kuvunja mkataba na kupambana nao nje ya uwanja.
“Viongozi kama watabaini ukweli wa nyuma ya Feisal kuna mtu anahusika kumrubuni mchezaji wetu, maana yake mtu huyu hana dhamira njema na Young African kama atakuwa mfanyabiashara, biashara yake kwa vyovyote vile sisi kama washabiki wa Yanga wanachama na wapenzi tunahusika katika kuinunua biashara yake hiyo. Hatuwezi kukubali kuona anatubomolea Yanga yetu halafu sisi tuendelea kuwa wateja wa biashara yake,” Kassim Mshamu, Mratibu Kanda ya Ilala.
Aidha, wamesema Azam si mara ya kwanza kuwachukua wachezaji wa Yanga pindi wanapokuwa na umuhimu zaidi katika klabu kwa kuwa walishafanya hivyo kwa baadhi ya wachezaji wa Yanga akiwemo Mrisho Ngasa, hivyo wamedai inawezakana huo ukawa mwendelezo.