Chama cha Watu Wenye Ualbino- TAS Wapata Msaada wa Vifaa.

0
36

Katibu Mkuu Chama cha Watu Wenye Ualbino Mkoa wa Dar Es Salaam Gaston Mcheka ametoa shukrani baada ya kupokea vifaa vya kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku.

Vifaa hivyo ni Mafuta maalum ya kutunza Ngozi, na kofia za kujikinga na mwanga wa jua ambavyo vyote hivyo vimetolewa kama msaada na Meridianbet Tanzania ikiwa ni sehemu ya kuwakumbuka watu mbalimbali wenye mahitaji tofauti kwenye jamii.

Akipokea vifaa hivyo Mcheka alibainisha kwamba Meridianbet imesaidia kwa kiasi kikubwa kwani vifaa hivyo vinagharama kubwa sana.

“Kiuhalisia haya mafuta yana gharama kubwa sana, ukichukua hii chupa moja ni gharama za chakula kwenye familia kwa milo mitatu, lakini leo hii wenzetu wa Meridianbet wametuletea vingi vya kutosha. Tunawashukuru sana kwa moyo hu una tutakuwa bega kwa began a Meridianbet kwa mambo mengine”- Gaston Mcheka

“Lakini mbali na hili nipende kuelezea tena changamoto ya kiyakinishi cha mezani au kiyakinishi mpakato ‘Laptop’ kwa ajili ya kufanyia shughuli zetu za kila siku hususani ya kutunza data zetu, ofisi yetu ni kubwa sna na mpya Serikali imejitahidi kutujengea ila hatuna vifaa mfano laptop, scanner, Kamera ili kuchukua matukio yetu”- Mcheka.

Nae Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Meridianbet Tanzania Matina Nkurlu alitoa neno lake kwa niaba ya kampuni.

“Sisi kama Meridianbet tumekuwa na desturi ya kuchangia kwa jamii bila kujali huyu ni nani, yule ni nani amezaliwa ana rangi ila kwakuwa ni Mtanzania sisi tunamsaidia kama ambavyo leo tumewatembelea Chama cha Watu Wenye Ualbino-TAS na kutoa vifaa vingi vya kuwasaidia kwenye Maisha yao”-Matina Nkurlu.

Pia aliongeza kwa kutoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano wa Meridianbet katika kusaidia jamii hususani watu wenye mahitaji maalum kama wenye Ualbino.

“Leo hii tumefarijika sana kufika hapa na kwa niaba ya Meridianbet nipende kusema kwamba tutawafikia watanzania wote popote pale walipo na tutaendelea kutoa misaada kwa jamii, hivyo nitumie nafasi hii kutoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano huu wa Meridianbet kwa kutoa msaada kwa ndugu zetu ambao wana matatizo mbalimbali”-Matina Nkurlu

Meridianbet ni kampuni inayojihusisha na michezo ya kubashiri kwa michezo mbalimbali bila kusahau michezo ya kasino mtandaoni ambayo inampa nafasi kila mtu ya kushiriki kirahisi na kujiweka kwenye nafasi ya kushinda pesa taslim na zawadi nyingi. Pia kwa kutambua ugumu wa Maisha na hali ya kila mmoja tumeamua kuweka mfumo wa kila mtu kubashiri bila bando wakati wowote mahali popote kwa kupiga *149*10# Bure kabisa.

Maisha ni utamaduni na desturi, hivyo Desturi ya Meridianbet ni kushirikiana na jamii kwenye kila jambo ambapo Chama cha watu wenye Ualbino-TAS wamepokea msaada wa vifaa kutoka Meridianbet kama Mafuta ya Ngozi, na kofia maalum za kujikinga na mwanga wa jua.

Bashiri na #Meridianbettz kwa kubonyeza hapa  https://app.mrdn.co/bashiri01

Send this to a friend