IMF: Mwaka 2023 utakuwa mwaka mgumu zaidi

0
22

Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Kristalina Georgieva amesema kwamba mwaka huu 2023 theluthi moja ya dunia itaathiriwa na mdororo wa uchumi.

Georgieva ameonya kuwa mwaka huu utakuwa mwaka mgumu zaidi ukilinganisha na mwaka jana kutokana na kudorora kwa uchumi wa Marekani, Umoja wa Ulaya (EU) na China.

Mnamo Oktoba mwaka huu, IMF ilipunguza mtazamo wake kwa mwaka 2023 katika ukuaji wa uchumi wa dunia, ikitoa mfano wa kuendelea kwa vita vya Ukraine pamoja na shinikizo la mfumuko wa bei na kuongezeka kwa kiwango cha riba na benki kuu.

New York yahalalisha miili kugeuzwa mbolea baada ya kifo

“Kwa miezi michache ijayo, itakuwa ngumu kwa nchi ya China, na athari ya ukuaji wa China itakuwa mbaya, athari katika eneo hilo itakuwa mbaya, athari katika ukuaji wa kimataifa itakuwa mbaya,” amesema.

Aidha, amesema kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 40 ukuaji wa kila mwaka wa China una uwezekano wa kuwa chini ya ukuaji wa kimataifa na kudhoofisha shughuli za kiuchumi duniani kote badala ya kuzisukuma hali ambayo haijawahi kutokea.

Send this to a friend