Mauzo ya nyama nje ya nchi yaongezeka kwa asilimia 21

0
22

Mauzo ya nyama nje ya nchi kwa kipindi cha Julai 15 hadi Desemba 15 mwaka jana yameongezeka na kufikia tani 5,158 sawa na ongezeko la asilimia 21.7, ikilinganishwa na tani 4,239 zilizouzwa katika kipindi kama hicho mwaka 2021.

Takwimu zimeonesha nchi inayoongoza kwa ununuzi wa nyama ikiwa ni Qatar ambao wamekwishanunua tani 504.

Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB), Dkt. Daniel Mushi amebainisha kuwa katika kipindi cha Novemba mwaka jana Tanzania iliuza nje ya nchi tani za nyama 1,423 zenye thamani ya dola za Marekani milioni 5.3, sawa na zaidi na TZS bilioni 10.

LATRA: Hakuna mwananchi atakayeshindwa kulipa ongezeko la nauli

Aidha, amesema kiasi hicho kilichouzwa ni sawa na ongezeko la asilimia 125 ikilinganishwa na tani 632 zilizouzwa Oktoba 2022.

“Tani 1,423 za nyama zilizouzwa Novemba mwaka Novemba mwaka 2022, ni sawa na ongezeko la asilimia 62 ikilinganishwa na tani 878 zilizouzwa Novemba mwaka 2021, mpaka hapo zimeongezeka tani 545,” amesema.

Send this to a friend