Urusi yatangaza kusitisha vita Ukraine kupisha sikukuu ya Krismasi

0
28

Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameamuru vikosi vyake kusitisha vita nchini Ukraine kwa saa 36 wiki hii ili kuwaruhusu Wakristo wa Orthodoksi kuhudhuria ibada ya Krismasi.

Maafisa wa Ukraine wametupilia mbali pendekezo hilo na kudai hizo ni njama za kutaka kupunguza mzozo huo unaoelekea mwaka wa pili

Mexico yasitisha kumpeleka mtoto wa El Chapo nchini Marekani baada ya watu 29 kuuawa

Agizo la Putin limekuja baada ya kiongozi wa Kanisa la Othodoksi la Urusi, Patriaki Kirill wa Moscow kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano kati ya Januari 6 na Januari 7, wakati ambao Wakristo wengi wa kanisa hilo husherehekea Krismasi kwa mujibu wa Kalenda wanayotumia inayojulikana kama kalenda ya Julian.

Wakati wa hotuba yake siku ya Alhamisi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema Urusi inalenga kutumia sikukuu hiyo kama kigezo cha kuzuia maendeleo ya Ukraine katika eneo la mashariki la Donbas.

Send this to a friend