Daktari bingwa kutoka Taasisi ya Mifupa (MOI) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Willium Mgisha amesema watu wanaovaa viatu vyenye visigino virefu kwa muda mrefu wako katika hatari ya kupata maradhi ya nyonga, mgongo na magoti.
Amebainisha kuwa binadamu akifikia umri wa miaka 40 anakuwa na mabadiliko ya mwili ikiwemo kuumwa miguu, magoti na nyonga maradhi ambayo baadhi husababishwa na uvaaji wa viatu virefu.
Dkt. Mgisha amefafanua kuwa mvaaji wa viatu vyenye kisigino kirefu kuanzia sentimeta nne hadi 10 yupo katika hatari zaidi kupata aradhi hayo.
“hatuwakatazi wanawake kuvaa viatu virefu kwa sababu ni moja ya urembo wao, ni kweli mwanamke akivaa kiatu cha aina hiyo anaonekana smati zaidi kuliko aliyevaa kiatu kifupi.
Utafiti: Wagonjwa wa moyo ambao hawajaoa wako hatarini zaidi kufariki
Lakini kiatu kirefu kinatakiwa kivaliwe kwa muda mfupi, isizidi saa mbili, halafu unabadilisha na kuvaa viatu vya kawaida,” ameeleza.
Aidha, amesema kwamba athari ya uvaaji wa viatu hivyo mara nyingi haijitokezi mapema ingawa tayari wameshapata kesi nyingi kuhusu maradhi hayo kwa vijana wadogo ambao wameathirika na tatizo hilo.