Chama cha Soka England chasema goli la Fernandes ni halali

0
27

Shirikisho la Soka England (FA) limesema hawakuona Rashford akiugusa mpira katika bao lililofungwa na mchezaji wa Manchester United, Bruno Fernandes kwenye mchezo dhidi ya Manchester City, hivyo linaunga mkono goli hilo ikiwa pia VAR haikuweza kupata ushahidi wa makosa ya wazi.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno aliirudisha Manchester United mchezoni dakika ya 78 baada ya kupata bao la kusawazisha kwa pasi ya Casemiro.

Casemiro alitoa pasi wakati Rashford akiwa kwenye eneo la kuotea, na alianza kukimbia kwenye uelekeo wa goli la Manchester City, lakini baada ya mikimbio michache aliuacha mpira huo, ndipo Fernandes alipiga na kufunga goli hilo.

Mwamuzi wa VAR, Stuart Atwell alitoa maamuzi kuwa lilikuwa goli halalai kwani Rashford hakugusa mpira wala hakuingilia kati mabeki wa Manchester City kwa nia ya kuwazuia kucheza mpira.

Hata hivyo hili limeibua mjadala kwani kwa mujibu wa sheria ya kuotea (offside), endapo mchezaji aliye kwenye nafasi ya kuotea atajaribu kuucheza mpira, basi itahesabika kwamba ameotea, tafsiri iliyofanya wengi kuamini kuwa goli la kwanza la Manchester United lilifungwa katika mazingira ya kuotea.

Dakika tatu tu baada ya kusawazisha, Rashford alifunga bao la ushindi kwa Mashetani Wekundu kwa pasi ya Alejandro Garnacho ambayo ilithibitisha pointi tatu muhimu kwa timu yake. Sasa wana pointi 38 baada ya kucheza mechi 18, wakiwa chini kwa pointi moja dhidi ya vijana wa Pep Guardiola.

Send this to a friend