Rais Ramaphosa asitisha safari ya Uswisi kutokana na mgao wa umeme
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amebatilisha mipango ya kuhudhuria Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) linakaofanyika huko Davos nchini Uswisi kwa sababu ya tatizo la umeme linaloendelea nchini mwake.
Nchi hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa zaidi la umeme kuwahi kutokea kutokana na matatizo katika shirika la umeme la nchi hiyo, Eskom, katika kipindi cha miezi 12 iliyopita hali inayopelekea umeme kukatika hadi saa sita kwa siku.
Ndege tatu za ATCL zasimamishwa kuendelea na kazi
Kwa mujibu wa Msemaji wa Rais, Vincent Magwenya amesema Ramaphosa alipaswa kuongoza wajumbe wa serikali kwenye hafla hiyo, lakini badala yake atafanya mazungumzo na viongozi wa vyama vya siasa na kampuni ya umeme inayomilikiwa na serikali ya Eskom.
“Rais Cyril Ramaphosa tayari amezungumza na uongozi wa Eskom na Kamati ya Kitaifa ya Mgogoro wa Nishati (NECCOM) na mikutano hiyo itaendelea,” amesema.