Ndugai: Tusihoji tu wajibu wa Serikali, wananchi pia tutekeleze wajibu wetu

0
23

Spika wa Bunge Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai ametoa wito kwa kila mwananchi kutekeleza wajibu wake katika kukuza maendeleo ya nchi badala ya kuiachia Serikali pekee yake.

Ndugai ameyasema hayo wakati akishirki mkutano wa kuutangazia umma mafanikio ya miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Sita katika mkoa wa Dodoma.

“Yako majukumu ya mtu binafsi, ya familia, ya jamii iliyoko pale ambayo hayo nayo yakifanyika, sasa yakiungana na yale ya Serikali ndio kinachoitwa maendeleo,” amesema.

CCM yawapa wiki moja mawaziri wa Elimu na TAMISEMI

Aidha, Ndugai ameeleza kuwa kila mmoja ana haki kikatiba na sababu ya kuhoji kinachofanywa na Serikali lakini pia wananchi wana wajibu wa kutekeleza majukumu yao kwa kufanya shughuli za kiuchumi ili kuisaidia Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Twendeni tukafanye shughuli za kiuchumi ni jukumu letu tukafuge kwa kadri tunavyoweza, Serikali kwa sababu ni baba na mama atatusaida majosho, kwa sababu siyo kila mtu ataweza kujenga josho lake, atatusaidia baadhi ya madawa na huduma nyingine za ugani,” ameeleza.

Send this to a friend