Sigara bandia za TZS milioni 573 zateketezwa

0
31

Kikosi cha kuzuia na kupambana magendo Kanda ya Ziwa kimeteketeza tani 13.25 za sigara bandia mkoani Shinyanga zilizokuwa zinaingizwa nchini.

Akizungumza wakati wa zoezi la kuteketeza sigara hizo zilizoteketezwa katika kichomea taka kilichopo kwenye Mgodi wa GGML mkoani Geita, Meneja Msaidizi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Forodha Mkoa wa Mwanza, Oswald Massawe amesema shehena hiiyo ina thamani TZS milioni 573.54.

Meneja wa Mamalaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa Magharibi (Geita), Dkt. Edgar Mahundi amesema sigara hizo zingetumika zingekuwa chanzo kikubwa cha magojwa mbalimbali ikiwemo saratani.

Send this to a friend