Kiongozi wa Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga ametangaza kuwa chama chake kamwe hakitoitambua serikali ya Rais William Ruto kutokana na madai kwamba hakuchaguliwa kihalali katika uchaguzi wa mwaka jana.
Katika hotuba yake leo Jumatatu Januari 23, 2023 katika bustani ya Kamukunji jijini Nairobi, Odinga ameendelea kushikilia kuwa Uchaguzi Mkuu wa Agosti 2022 uliibiwa ili kumpendelea Dkt Ruto hivyo serikali ya Kenya iko madarakani kinyume cha sheria.
“Kwanza, sisi kama Azimio tunakataa matokeo ya uchaguzi wa 2022. Hatuwezi na hatutatambua utawala wa Kenya Kwanza na tunachukulia serikali ya Kenya Kwanza kuwa haramu,” amesisitiza Odinga.
Misri yawataka raia wake kula miguu ya kuku kutokana na mfumuko wa bei
Aidha, Raila Odinga ametamka kuwa anataka Rais Ruto na viongozi wote katika serikali ya Kenya Kwanza kujiuzulu kwa kuwa haina mamlaka wala uwezo wa kutawala nchi hiyo.
Ameongeza kuwa rekodi zote za uchaguzi wa 2022 katika Tume ya Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ziwekwe hadharani na kukaguliwa na chombo kisichoegemea upande wowote kwa kuwa ukaguzi wa kimahakama wa matokeo hayo pamoja na IEBC hauwezi kuaminiwa.