Rwanda: Waziri mstaafu ahukumiwa miaka 5 jela kwa ufisadi

0
13

Mahakama Kuu mjini Kigali nchini Rwanda imemhukumu kwenda jela miaka mitano pamoja na kulipa faini ya Rwf30 milioni [TZS milioni 65.1] aliyekuwa waziri wa utamaduni wa Rwanda, Edouard Bamporiki (39) kwa madai ya rushwa.

Uamuzi huo umefuata baada ya mshitakiwa kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa Septemba mwaka jana, ikimhukumu kwenda jela miaka 4 kwa makosa ya kutumia vibaya mamlaka aliyopewa.

Rais Paul Kagame alimfukuza kazi Bamporiki mwezi Mei mwaka jana kabla ya waendesha mashitaka kutangaza kufanya uchunguzi juu yake kuhusu matumizi mabaya ya madaraka na kuomba rushwa ya thamani ya Rwf 5milioni [TZS milioni 10.9] kutoka kwa mfanyabiashara kwa ahadi ya kumsaidia kufungua tena kiwanda chake cha pombe kilichofungwa.

Kainerugaba: Nitakuwa rais wa Uganda baada ya baba yangu

Mbali na hayo, anadaiwa kupokea hongo yenye thamani ya Rwf milioni 10 [TZS milioni 21.8] kutoka kwa mtu huyo huyo, na kuahidi kumsaidia kumtoa mke wake kutoka mikononi mwa Polisi ambaye alikuwa akikabiliwa na mashitaka yanayohusiana na ufisadi wakati huo.

Bamporiki alikiri mashitaka hayo kwenye mtandao wa Twitter na kumuomba Rais amsamehe, lakini mnamo Septemba mahakama ya mwanzo ilimhukumu kifungo cha miaka minne, ambapo alikata rufaa.

Send this to a friend