Mahakama yaamuru binti kulipa fidia kwa kumkataa mchumba aliyemsomesha

0
50

Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Fortunate Kyarikunda wa nchini Uganda ameamriwa na mahakama kumlipa fidia aliyekuwa mchumba wake baada ya kulipiwa ada ya chuo na kisha kumuacha .

Mahakama ya Kanungu imesema katika uchumba huo uliodumu kwa miaka minne, Richard Tumwine alilipa TZS milioni 5.9 kwa ajili ya masomo ya mchumba wake ya sheria, na kwamba binti huyo amevunja ahadi kwa Tumwine.

Aidha, mahakama imedai haikuwa sawa kwa mshitakiwa kutumia ulaghai kwa kusema kwamba wazazi wake walimwambia asiolewe na mwanaume mzee, kwa kuwa alikuwa na nafasi ya kukataa maombi ya Tumwine toka awali.

Ndoa yavunjwa baada ya mke kunyimwa tendo la ndoa kwa miaka saba

Hata hivyo baadhi ya wakosoaji wamedai hukumu hiyo ina dosari kwa sababu ulikuwa ni uchumba, na kwamba uchumba ni tofauti na ndoa.

Wakati huo huo, Kikundi cha Utetezi wa Wanawake cha ED EASSI kimedai kuwa wakati mwingine kuna mazingira ya kinyonyaji kwa wanawake ambapo mwanaume hutoa pesa kwa mwanamke kwa sharti la kumuoa.

Send this to a friend