Kampuni ya Adani yakanusha ripoti iliyotolewa na Marekani

0
16

Shirika la Kimataifa la India limesema ripoti ya madai iliyotolewa dhidi ya makampuni yake na Taasisi ya Utafiti ya Hindenburg yenye makao yake New York nchini Marekani ni ya uongo.

Katika majibu yake, kampuni ya Adani Group imesema kuwa ripoti ya Hindenburg yenye kurasa 106 iliishutumu kampuni kwa udanganyifu wa hisa na udanganyifu wa kimahesabu hali iliyotafsiriwa kuwa ni mashambulizi dhidi ya kampuni.

“Hili sio tu shambulio lisilo la lazima kwa kampuni yoyote mahususi lakini ni shambulio la kimahesabu kwa India, uhuru, uadilifu, ubora wa taasisi za India, na matarajio ya India,” imesema Adan Group ambayo inamilikiwa na Gautama Adani.

Kwa mujibu wa taarifa, ripoti ya kampuni ya New York imepelekea kampuni ya Adani Group kupoteza zaidi ya dola bilioni 50 [TZS trilioni 117] za thamani ya soko katika vikao viwili tu vya biashara na mmiliki wa Adani, Gautam kupoteza zaidi ya dola bilioni 20 [TZS trilioni 47] au karibu moja ya tano ya utajiri wake wote.

Mwigizaji Idris Elba kufungua studio ya filamu nchini

Kampuni ya Adani Group kwa Tanzania kupitia Adani Ports na Special Economic Zone Limited imepewa kandarasi ya kuwa mtoa huduma wa kuhudumia makontena pembezoni mwa Bandari ya Dar as Salaam ambapo awali ilikuwa inasimamiwa na Tanzania International Container Terminal Services (TICTS).

Hapo jana maofisa wa bandari walisisitiza kuwa Adani Group ilikuwa inafanya kazi tu kama mtoa huduma ambaye analipwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) mwishoni mwa mwezi.