Kuzungumza mbele ya watu wengi inaweza kuwa si jambo rahisi kwa watu wengi, iwe ni shuleni, kwenye harusi mkutanoni n.k.
Vidokezo hivi vitakusaidia kuondokana na hofu na kuzungumza pasipo uoga;
Fanya maandalizi
Jiweke tayari na ujipange kwa ajili ya wasilisho lako, kwani utajiweka kwenye nafasi nzuri ya kufanya vizuri na kuepuka baadhi ya mambo kwenda kombo. Unaweza kufanya mambo haya;
• Tembelea ukumbi au chumba utakachowasilisha wasilisho lako mapema.
• Hakikisha unachapisha kila kitu unachohitaji angalau siku moja kabla
• Jitayarishe kwa hitilafu zozote za kiufundi ikiwemo kuwa na nakala ngumu endapo video uliyoiandaa haitacheza
• Fika mapema eneo utakalowasilisha wasilisho lako
Kuwa na mawazo chanya
Fikiria namna ambavyo utatoa wasilisho lako kwa ujasiri na kwa mafanikio kwani hii itaimarisha imani yako.
Fanya mazoezi
Ikiwa una muda, fanya mazoezi kabla. Mazoezi hutoa ‘endorphins’ ambayo hupunguza viwango vya ‘stress’ yako na kukufanya ujisikie vizuri.
Pia unapaswa kufanya mazoezi ya kile utakachokwenda kukiwasilisha, kwani ukifahamu zaidi unachokiwasilisha hadhira yako itakuona kuwa unajiamini.
Vidokezo vya kufanya mazoezi:
• Usisome tu kilichoandikwa, simama na useme kwa sauti kana kwamba unawasilisha kwa hadhira
• Hakikisha unafanya mazoezi ukihusisha lugha ya mwili wako zikiwemo ishara za mwili
• Fanya mazoezi mbele ya wengine na upate maoni yao.
Ondoa hofu
Kumbuka kwamba hujaalikwa kuzungumza ili wakudhihaki, hadhira inataka kukusikia ukizungumza. Dhibiti uoga na wasiwasi wako kwa kuepuka kutumia kafeini nyingi kabla ya tukio, kwani hiki ni kichocheo na kinaweza kukufanya kuwa na wasiwasi na kutetereka.
Sikiliza muziki
Tayarisha idadi ya nyimbo ambazo unaweza kusikiliza ukiwa njiani kuelekea kwenye tukio. Hakikisha nyimbo utakazoandaa zitakupa msukumo zaidi kwenye jambo unalokwenda kufanya.