Mambo ya msingi ya kufahamu unapotaka ku-verify akaunti ya Twitter

0
31

Baada ya mfanyabiashara Elon Musk kuichukua Twitter, amefanya mabadiliko makubwa katika mtandao huo ikiwemo mabadiliko kwenye Twitter Blue ambayo ina vipengele vipya na yenye gharama.

Twitter Blue inawapa watumiaji vitu viwili; kuipa akaunti mvuto kwa kuongeza alama ya tiki ya bluu au dhahabu (kwa biashara), pamoja na kunufaika na baadhi ya vipengele ambapo watumiaji wanapaswa kuvilipia ada ya kila mwezi ya $11 (TZS 25,723) kwa watumiaji wa iOS na $8 (TZS 18,708) kwa watumiaji wa wavuti.

Hivi ni baadhi ya vipengele wanavyoweza kufaidika watumiaji wa Twitter Blue;

Ku-edit
Kipengele cha uhariri (edit) kimeombwa kwa muda mrefu. Watumiaji watafurahia ku-edit tweets zao mara nyingi watakavyo ndani ya dakika 30 za mwanzo.

Mahudhui
Ikiwa unatumia twitter ili kupata maudhui kama habari, basi unaweza kuzifikia makala zinazojadiliwa zaidi.

Video ndefu
Unaweza kupakia video za dakika sitini katika ubora ang’avu 1080p kwenye Twitter Blue. Hii ni muhimu sana kwa watengenezaji wa maudhui, biashara na watu mashuhuri wanaotumia twitter kama sehemu yao kuu ya mawasiliano.

’Bookmark folder’
Kipengele hiki kinaweza kuwa muhimu katika kuhifadhi tweets zako za muhimu kwenye kumbukumbu ili uweze kuzipata kwa urahisi siku zijazo.

Fahamu faida 5 za kunywa maji ya moto asubuhi

Licha ya sifa hizo kuna mambo machache mbayo yanaweza kuwachukiza watumiaji;

Mahitaji ya namba ya simu
Akaunti yako lazima iunganishwe na namba yako ya simu kabla ya kuthibitishwa, jambo linaloweza kuhatarisha usalama binafsi.

Matangazo
Twitter Blue haiondoi matangazo, jambo ambalo linaweza kuwakera watumiaji.

Watumiaji wanaahidiwa kuwa wataona matangazo machache ambayo ni kwa asilimia 50. Ikiwa unalipia huduma hii, je matangazo yanapaswa kuwa sehemu ya huduma?

Send this to a friend