Arteta ataka Arsenal irejeshewe pointi 2 kwa makosa ya VAR

0
36

Kocha wa klabu ya Arsenal, Mikel Arteta amedai ataridhika endapo timu yake itarudishiwa pointi mbili kutokana na makosa ya VAR ambayo yaliruhusu bao la kusawazisha la Brentford kwenye mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu ya England.

Bodi ya waamuzi, PGMOL imeomba radhi kwa klabu ya Arsenal baada ya kulaumiwa kwa uamuzi usio sahihi wa VAR, ikidai ni makosa ya kibinadamu.

Arteta amedai haikuwa makosa ya kibinadamu na kwamba jambo hilo halikubaliki.

“Iliigharimu Arsenal pointi mbili ambazo hazitarejeshwa, kwa hivyo itabidi tupate pointi hizo mbili mahali pengine kwenye ligi,” amesema.

Rais Samia kununua kila goli la Simba na Yanga kwa TZS milioni 5

Hata hivyo, Afisa Mkuu wa Waamuzi wa PGMOL, Howard Webb amewasiliana na Klabu ya Arsenal ili kukiri na kueleza makosa hayo yaliyotokea.

Naye Refa wa zamani wa EPL, Webb ambaye alichukua jukumu hilo mwishoni mwa mwaka jana, pia ameomba msamaha kwa klabu ya Brighton baada ya bao lililokataliwa kwa kuotea dhidi ya Crystal Palace Jumamosi, kwa sababu miongozo ya VAR ilitolewa kimakosa.

Send this to a friend