Uwanja wa Benjamin Mkapa kufungwa

0
31

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeshauri kutotumika kwa uwanja wa Benjamini Mkapa uliopo jijini Dar es Salaam katika mechi zao wakidai umeharibika katika eneo la kuchezea (pitch) hivyo kufungwa kwa mwezi mmoja kwa ajili ya marekebisho baada ya mechi ya Yanga SC dhidi ya KCMC Jumatano Februari 22, 2023.

Kwa mujibu wa Meneja wa Uwanja huo, Salum Mtumbuka, baada ya mechi mbili za CAF zilizochezwa wikiendi iliyopita walikutana na maofisa hao ambao waliwapa maelekezo namna ya kufanya marekebisho hasa kwenye eneo la kuchezea.

“Tulikubaliana kwa pamoja na CAF wakati marekebisho yanaendelea ambayo yatachukua muda wa mwezi mmoja, mechi zitakazochezwa hapo hapo labda ni zile za kimataifa za CAF na timu ya Taifa, mechi zingine za Ligi Kuu wanaotumia uwanja huu watatafuta viwanja vingine hata Uhuru upo [Uwanja wa Uhuru],” amesema.

Eng. Hersi: Feisal bado hajarudi kambini, anadanganywa

Ameongeza, “Simba na Yanga ndiyo wanaotumia huu uwanja kama uwanja wao wa nyumbani, ila ndani ya kipindi cha marekebisho haya hawatatumia mechi zao za Ligi Kuu kwenye uwanja huu, tunawapa uwanja wa Uhuru ama watakavyoona wao.”

Hata hivyo Mtumbuka amedai kwa matumizi ya uwanja huo ni kwamba ndani ya wiki moja zinatakiwa kuchezwa mechi tatu tu yaani siku tatu, lakini sasa uwanja huo umetumika sana kinyume na matumizi yanayotakiwa.

Chanzo: Mwanaspoti

Send this to a friend