Waziri Nape: Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi Tanzania 

0
22

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema mfanyabiashara, Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi ya Starlink nchini katika hatua yake ya kuwekeza katika utoaji wa huduma ya intaneti kupitia satelite.

Akizungumza na ITV Waziri Nape amesema mpango wa Elon Musk ulikuwa ni kuweka ofisi nchini Marekani hali ameielezea kuwa ingeweza kuleta usumbufu pale ambapo wateja wangehitaji msaada zaidi.

“Kwenye mipango yao walikuwa hawana mpango wa kuweka ofisi hapa, sasa mimi nawauliza ikitokea fault (tatizo) yoyote hawa wateja wenu mnataka waje ofisini kwangu? Wekeni ofisi hapa, mnawekaje ofisi Marekani? Hawa Waswahili mnaowahudumia watapiga simu Marekani walalamike kwamba mbona nimelipa sijapata bando langu, mtaniletea mimi shida,” amehoji.

Aina 5 ya mazungumzo ambayo hutakiwi kuyafanya kupitia ukumbe wa maandishi

Aidha, amesema jambo lingine ambalo hawakuorodhesha katika mpango wao  ni jinsi gani wataweza kulinda data wanazozikusanya kutoka kwa wateja wao na wapi zinakwenda.

Hivi karibuni kupitia mtandao wa Twitter biliobea Musk alisema anasubiri kibali cha Serikali kuwekeza nchini, lakini Waziri Nape alimjibu kuwa Serikali nayo inasubiri awasilishe nyaraka alizotakiwa kuambatanisha kama sehemu ya maombi.

Send this to a friend