Meridianbet kama ilivyokua desturi yao ya wa miaka yote ni kujitahidi kile wanachokipata basi wanarudisha katika jamii ambayo inawazunguka hasa wale watu ambao wana uhitaji zaidi, Meridianbet ilifunga safari mpaka Temeke na kutembelea klabu ya soka ya watu wenye ulemavu inayofahamika kwa jina la Parasports Club na kutoa msaada wa vifaa vya michezo.
Parasports Club ni timu ya mpira wa miguu ya watu wenye ulemavu ambayo inatambulika rasmi na Meridianbet Tanzania waliona moja ya sehemu ambayo wanaweza kuigusa jamii wakati huu basi Parasports Club na kwenda kutoa msaada ambao utawasogeza kwa namna moja ama nyingine.
Timu ya Merdianbet ilifika Temeke ikiongozwa na mkuu wa kitengo cha masoko Bwana Matina Nkurlu akiwa na msaidizi wake Twaha Ibarahim walifanikiwa kutoa vifaa vya michezo kama ifuatavyo Jezi jozi moja, Bibs jozi moja, Mipira minne, pamoja na sare za viongozi wa timu ya Parasports Club.
Timu ya Meridianbet ikiongozwa na wana Matina Nkurlu ilipata fursa ya kuzungumza na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo ambao kwa kiasi kikubwa walionesha kushukuru kwa kile ambacho mabingwa wa michezo ya kubashiri Meridianbet wamekifanya kwao, Vilevile Viongozi wa Parasports Club hawakuacha kutoa shukrani zao za dhati kwa Meridianbet baada ya kupokea msaada huo.
Bwana Matina Nkulu mkuu wa kitengo cha Masoko na mawalisiliano ndani ya Meridianbet naye hakuacha kushukuru kwa mapokezi ambayo ameyapata ndani ya Parasports club inayopatikana wilayani Temeke na kuahidi kuendeleza hichi walichokifanya leo ndani ya Paraspots Club, Huku pia akisema inawezekana wakapata wasaa wa kuitembelea tena klabu hiyo kutokana na mapokezi mazuri waliyoyapata.
Naibu Afisa Masoko ndani ya Meridianbet Bwana Twaha Ibrahim amesema licha ya wao kua mabingwa na wakongwe katika michezo ya kubashiri ambayo unaweza kubashiri na kushinda mamilioni kupitia michezo ya Casino, na michezo mpira wa miguu kutoka ligi mbalimbali barani ulaya, Lakini hichi walichokifanya leo ndio sehemu wanayotumia kuhakikisha wanarudisha kile kidogo wanachopata katika jamii inayowazunguka.