Fei Toto apeleka TFF ombi kuvunja mkataba na Yanga

0
17

Mchezaji wa Klabu ya Yanga, Feisal Salum (Fei Toto) amefika katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) akiwa na mwakilishi wake Jamsin Razack kuwasilisha maombi yake mapya ya kuvunja mkataba kati yake na Yanga.

Hatua hiyo imefuata baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania  (TFF) kutupilia mbali shauri la mchezaji  huyo baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili.

Akizungumza mwakilishi wake, Jamsin Razack amesema ana imani mchezaij huyo atapata haki yake kutoka TFF kwa kuwa ndio chombo pekee kinachoweza kuvunja mkataba baina ya mchezaji na klabu yake.

TFF imemtangaza Adel Amrouche kuwa kocha mkuu Taifa Stars

“Feisal kaleta ombi la kuomba kuvunja mkataba wake na Yanga, hili ombi limepokelewa, tuwaachie TFF watatoa maamuzi  [..]. Nina imani na TFF ni chombo cha mpira, hapa ndio patakapotoa uamuzi.

Aidha ametoa wito kwa wachezaji nchini kusoma na kuzielewa kanuni zilizopo kabla ya kuchukua maamuzi yoyote.

Mbali na hayo, amewaomba wadau mbalimbali kutoa taarifa sahihi bila kuichafua TFF kwa kuwa kinachochafua mpira wa Tanzania kinaichafua nchi kwa ujumla.

Send this to a friend