Lema apewa siku saba kuwaomba radhi bodaboda

0
44

Chama cha Waendesha Pikipiki na Wamiliki wa Pikipiki Tanzania (CHAMWAPITA) kimemtaka aliyewahi kuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kufuta kauli yake aliyosema kuwa bodaboda ni ‘kazi ya laana.’

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga Mwenyekiti wa chama hicho, Michael Haule amesema chama hicho kimetoa siku saba kwa mwanasiasa huyo kurudi kwenye vyombo vya habari na kuwaomba radhi bodaboda wote, na kwamba endapo hatofanya hivyo chama hicho kinakusudia kufanya maandamano nchi nzima kupinga kauli za namna hiyo zinazotolewa na wanasiasa.

“Kazi hii ni kazi rasmi, imerasimishwa mwaka 2011 tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria ndio maana unakuta sisi kama maafisa wasafirishaji tunaishi kama wanavyofanya kazi wengine [..] anaposema kazi hii imelaaniwa, ametukashifu pakubwa sana,” amesema mwenyekiti.

Bashe aagiza Dkt. Mshindo Msola akamatwe

Ameongeza kuwa “tunalitaka Jeshi la Polisi, matamko kama haya yanayochonganisha kati ya taasisi na vyama vya upinzani wayakemee, na kama hawatayakemea sisi tumeamua sasa tuyakemee kwa nguvu zote, kwa nguvu zote ambazo tutajaliwa na mwenyezi Mungu.”

Send this to a friend