Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetangaza kupungua kwa mfumuko wa bei nchini kutoka asilimia 4.9 kwa mwaka ulioishia Januari, 2023 hadi kufikia asilimia 4.8 kwa mwaka ulioishia Februari.
NBS imesema kupungua kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwaka ulioishia Februari 2023 kumechangiwa na kupungua kwa mfumuko wa bei kwa baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula ikilinganishwa na Januari 2023.
Baadhi ya bidhaa zilizoonesha kupungua bei ni pamoja na ngano kutoka asilimia 7.7 hadi 7.1, dagaa wakavu kutoka asilimia 5.7 hadi asilimia 1.1 na vinywaji baridi kutoka asilimia 14.0 hadi asilimia 12.7.
Ajali: Polisi kukagua shule za udereva na namna madereva walivyopata leseni
Aidha, bidhaa zisizo za vyakula zilizoonesha kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na bidhaa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa nyumba kutoka asilimia 7.9 hadi asilimia 5.0, gesi kutoka asilimia 9.7 hadi asilimia 9.1, mafuta ya taa kutoka asilimia 36.9 hadi asilimia 33.1, dizeli kutoka asilimia 33.1 hadi asilimia 27.8 pamoja na bidhaa na huduma kwa ajili ya usafi binafsi kutoka asilimia 4.2 hadi asilimia 3.7.
“Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioshia mwezi Februari, 2023 umepungua hadi asilimia 9.6 kutoka asilimia 9.9 kwa mwaka ulioshia mwezi Januari, 2023,” imeeleza taarifa