Wachimbaji 8 wafariki kwa kufukiwa na kifusi Geita

0
15

Wachimbaji nane wamefariki dunia katika Kijiji cha Igando, Kata Magenge Halmashauri ya wilaya ya Geita mkoani Geita baada ya kufukiwa na kifusi cha mgodi usiku wa kuamkia leo wakati wakichimba madini.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi wa Polisi, Safia Jongo amesema watu hao walivamia katika eneo hilo lililokuwa limezuiliwa na kuanza shughuli ya uchimbaji bila kufata taratibu.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Geita, Shabani Dawa amesema walifika katika eneo la tukio majira ya usiku ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kutoa miili ya watu 8.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela amepiga marufuku shughuli za uchimbaji katika maeneo ambayo sio rasmi kwani yanahatarisha maisha kutokana na kufanya shughuli hizo kinyume na sheria na kusababisha maafa kwa wananchi.

Mume adaiwa kumuua mkewe na kumzika chumbani

Afisa Madini Mkoa wa Geita Martine Shija amesema eneo hilo lilikuwa ni eneo lenye leseni ya utafiti ambapo lilikuwa limezuiliwa kufanya shughuli za uchimbaji na wachimbaji hao wameingia na kuanza kufanya uchimbaji kinyume na sheria.