Fahamu aina 3 za machozi aliyonayo binadamu na kazi zake

0
65

Kwanini binadamu hulia?
Hisia zako zinaweza kukufanya ulie ukiwa na huzuni, hasira au furaha. Kulia kwa sababu za kihisia kunaweza kukufanya ujisikie vizuri, hutoa mvutano na kusaidia akili yako kuanza upya.

Je! Unajua kuwa kuna aina mbalimbali za machozi? Hizi ni aina 3 za machozi hayo;

1. Machozi kinga (Basal tears)

Haya ni machozi ambayo hutolewa mfululizo kwa kiasi kidogo ambapo huwa ndani ya macho muda wote ili kulainisha konea na kuiweka safi dhidi ya vumbi. Machozi haya husaidia macho kupambana na maambukizi. Unapopepesa macho husambaa juu ya uso wa jicho lako ili kuboresha kuona kwako. Machozi ya haya hupambana dhidi ya maambukizi ya bakteria kama sehemu ya mfumo wa kinga.

Namna 5 ya kuepuka kupatwa na kiharusi

2. Machozi ya kujisafisha (Reflex tears)

Haya ni machozi ambayo macho yako hutoa wakati unapokata vitunguu, moshi, mabomu ya machozi, yanapoingiwa mdudu au pilipili. Machozi haya hutolewa kwa kiasi kikubwa zaidi kuliko machozi kinga ambayo pia yamebeba kinga mwili ili kusaidia kupambana na vijidudu.

3. Machozi ya kihisia (Emotional tears)

Haya ni machozi yanayokutoka unapopitia jambo fulani linalohusisha hisia za aina zote kama hasira, mateso, maombolezo, furaha sana au vicheko vikali. Yana protini na homoni za ziada ambazo huwezi kupata katika machozi mengine kama vile prolactini, potasiamu, manganese na homoni za mafadhaiko.

Nadharia moja ya kwa nini tunalia machozi ya hisia ni kwamba unatoa mkazo (stress) kupitia machozi ili kusaidia kutuliza mwili wako.

Machozi ya hisia hutumwa ili kutoa utulivu haraka, pia yanajumuisha athari za kimwili kama vile kuongezeka kwa mapigo ya moyo na kupumua polepole.